Pages

Ads 468x60px

Tuesday, August 5, 2014

XAVI ATANGAZA KUSTAAFU KUITUMIKIA TIMU YA TAIFA.




                                          Xavi Hernandez.

Kiungo wa timu ya Fc Barcelona Xavi Hernandez ametangaza rasmi kustaafu kuchezea timu ya taifa lake la Hispania tangu acheze mchezo wa kwanza na mabingwa hao wa zamani wa dunia mwaka 2000 akiwa na umri wa miaka 20.
Xavi mwenye umri wa miaka 34 katika mkutano wake na waandishi wa habari leo jumanne amesema alitaka kustaafu baada ya kumalizika kwa fainali za kombe la mataifa ya Ulaya mwaka 2012 lakini kocha Vicente Del Bosque alimzuia.
Akiwa amecheza michezo 133 kwenye timu yake  ya taifa nakufunga magoli 13 amewashukuru mashabiki,wachezaji na viongozi wa shirikisho la soka la Hispania kwakumuunga mkono muda wake wote alikuwa kwenye timu ya taifa.
Tangu aanze kuichezea timu ya taifa Xavi amefanikiwa kushinda kombe la dunia mara moja,kombe la mataifa ya Ulaya mara mbili huku akichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mashindano ya mataifa ya Ulaya mwaka 2008.
                               Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment