Pages

Ads 468x60px

Wednesday, August 20, 2014

MODRIC AJIPIGA KAMBA NNE REAL MADRID.



Kiungo ya Real Madrid raia wa Croatia Luka Modric amesaini mkataba mpya wa miaka minne kuendelea kubakia kwa mabingwa hao wa Ulaya kwa upande wa vilabu hadi mwaka 2018.
Real madri kupitia tovuti yake imetangaza Modric kurefusha mkataba wake utakaomfanya aendelee kusalia Santiago Bernabeu tangu ajiunge nayo mwaka 2012 akitokea Tottenham Hotspurs.

Modric mwenye umri wa miaka 28 amecheza michezo 67 katika ligi kuu ya Hispania maarufu kama La Liga na licha ya kukabiliwa na ugumu kwenye msimu wake wa kwanza kwasasa kiungo huyo amekuwa msaada mkubwa kwenye nafasi ya kiongo ya Real Madrid.
                               Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment