Pages

Ads 468x60px

Wednesday, August 6, 2014

LIVERPOOL MWENDO MDUNDO KWENYE USAJILI YANASA SAINI YA KINDA WA KIHISPANIA.




                                                     Javier Manquillo.

Timu ya soka ya Liverpool ya nchini England imeendelea kuimarisha kikosi chake katika msimu huu wa usajili baada ya kufanikiwa kumsajili kwa mkopo mlinzi wa pembeni kutoka kwa mabingwa wa ligi kuu ya Hispania Atletico Madrid Javier Manquillo.

Manquillo mwenye umri wa miaka 20 yupo katika kikosi cha timu ya taifa ya Hispania ya vijana wenye umri wa miaka ishirini mara baada ya kukamilisha uhamisho huo amesema anajisikia furaha kujiunga na vijogoo hao wa Anfield.

Raia huyo wa Hispania amebainisha kuwa anaamini Liverpool ni mmoja ya vilabu vikubwa barani Ulaya ambayo kila mchezaji anatamani kuichezea hivyo atahakikisha anaonyesha kipaji chake.

Manquillo anakuwa mchezaji wa saba kusajiliwa na kocha Brandan Rodgers msimu huu akiungana na Rickie Lambert, Adam Lallana, Emre Can, Lazar Markovic, Dejan Lovren  na  Divock Origi.
                                 
                          Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment