Pages

Ads 468x60px

Monday, July 14, 2014

MANCHESTER UNITED YALAMBA MKATABA MNONO WA MIAKA 10 KWA KAMPUNI YA ADIDAS.



                      kikosi cha Manchester United.

Mabingwa mara 20 wa ligi kuu ya England timu ya Manchester United imefikia makubaliano na kampuni ya Adidas kwaajili ya kutengeneza vifaa vyao vya michezo kwa mkataba wa miaka 10.

Taarifa kutoka katika tovuti ya timu hiyo kongwe barani Ulaya na dunia kwa ujumla imethibitisha uwepo wa makubaliano hayo ambapo udhamini huo ni wa thamani ya paundi milioni mia saba na hamsini na unataraji kuanza msimu wa 2015/2016.

Udhamini huo umevunja rekodi ya udhamini uliopita wa kampuni ya Nike ambao ulimalizika mwezi wa nne mwaka huu na makubaliano ya kampuni hiyo ya Nike kutengeneza vifaa vya Manchester United yanaishia mwezi huu wa saba.

Wakati huohuo kocha mpya wa  Manchestwer United Louis Van Gaal anataraji kuanza kazi ya kuifundisha timu jumatano ya wiki hii baada ya kumalizika kwa fainali za kombe la dunia ambapo kocha huyo ameeisaidia Uholanzi kushika nafasi ya tatu.

                   Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment