Pages

Ads 468x60px

Saturday, July 12, 2014

ARGENTINA YAADHIBIWA NA FIFA.








Shirikisho la Soka Duniani-FIFA limeitoza timu ya taifa ya  Argentina faini ya dola 336,000 kwa kushindwa kupeleka wachezaji katika mikutano minne ya wanahabari katika michuano ya Kombe la Dunia.

Kamati ya nidhamu ya FIFA imedai kuwa Argentina wamekiuka taratibu za vyombo vya habari na masoko katika mikutano ya kabla ya mchezo kuanza kwenye michezo dhidi ya Nigeria, Uswis, Ubelgiji na Uholanzi ambayo kocha pekee alikuwa anafika bila mchezaji ikiwa ni kinyume na sheria za soka. 

 Argentina watavaana na Ujerumani katika fainali ya michuano hiyo hapo kesho, lakini mpaka hivi sasa hawajatoa kauli yoyote ya kama wanakubali au kukata rufani kutokana na adhabu hiyo waliyopewa.

Hata hivyo michuano ya kombe la dunia leo inaendelea nchini Brazil,ambapo wenyeji wa michuano hiyo watakabiliana na Uholanzi ili kumtafuta mshindi wa tatu.

                       Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment