Pages

Ads 468x60px

Sunday, July 13, 2014

BABU ALIYEIFIKISHA ALGERIA ROBO FAINALI YA KOMBE LA DUNIA ATUA Trabzonspor YA UTURUKI.




                   Vahid Halilhodzicakitoa maelekezo kwa nyota wa Algeria.

Timu ya soka ya Trabzonspor inayoshiriki ligi kuu ya Uturuki imemteua  aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Algeria Vahid Halilhodzic kuwa kocha wao mkuu.

Vahid mwenye umri wa miaka 61 aliiongoza vyema Algeria nakufikia hatua ya robo fainali kwenye michuano ya kombe la dunia inayofikia tamati usiku huu nchini Brazil kwakuchezwa mchezo wa fainali baina ya Argentina na Ujerumani.

Kocha huyo ambaye alijiuzulu mara baada ya Algeria kuondoshwa na Ujerumani  kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la dunia hii ni mara yake ya pili kuinoa timu hiyo baada ya kuifundisha mwaka 2005.

Hata hivyo kocha huyo ambaye mkataba wake haujawekwa wazi ni wa muda gani amewahi kuvifundisha mataifa  mbalimbali ikiweno  Croatia, France, Ivory Coast, Morocco na Saudi Arabia.

                                    Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment