Pages

Ads 468x60px

Monday, July 28, 2014

IVORY COAST KATIKA VITA YA KUMSAKA KOCHA MPYA WA TIMU YA TAIFA.






Wakati shirikisho la soka nchini Ivory Coast likitarajia kumtangaza kocha mpya wa timu ya taifa ya nchi hiyo,
Kocha Mfaransa Herve Renard ametajwa katika orodha ya mwisho ya kuwania nafasi ya kukinoa kikosi hicho.

Orodha hiyo imetolewa na Shirikisho la Soka la nchi hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo makocha watatu wametajwa huku mshindi wa nafasi hiyo akitarajiwa kutangazwa mwishoni mwa mwezi huu wa julai.

Renard ambaye aliiongoza timu ya taifa ya Zambia maarufu kama Chipolopolo kushinda kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2012 anakabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa Mfaransa mwenzake Frederic Antonetti ambaye ameifundisha Rennes.

Hata hivyo kocha wa zamani wa Sporting Lisbon na Benfica Jose Manuel De Jesus wa Ureno ni miongoni mwa makocha wa wanaotarajiwa kuhojiwa na kamati ya utendaji ya shirikisho hilo kabla ya uamuzi wa mwisho.
                          Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment