Pages

Ads 468x60px

Sunday, July 13, 2014

SCOLARI: HATMA YA KIBARUA CHANGU IPO MIKONONI MWA FA YA BRAZIL.



Baada ya Brazil kupokea kipigo cha magoli 3 kwa 0 mbele ya Uholanzi usiku wa kuamkia leo kwenye mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu katika fainali za kombe la dunia kocha  Luiz Flipe Scolari amesema hatima yake ipo mikononi mwa  FA ya nchi hiyo.

Kocha huyo mwenye umri wa  wa miaka 65 amesema mkataba wake unamalizika mara baada ya kuisha kwa fainali za kombe la dunia lakini kulikuwa kunamapendekezo ya kuendelea na kazi kama itawezekana.

Scolari ambaye aliiongoza Brazil kushinda kombe la dunia mwaka 2002 amesema suala la kuendelea na kibarua cha kuifundisha timu hiyo lipo mikononi mwa raisi wa shirikisho la soka la Brazil na bodi yake nay eye atawasilisha taarifa yake ya mashindano  mezani kwao.

Mchezo wa  usiku wakuamkia leo ulikuwa wapili kufungwa mfululizo baada ya jumanne ya wiki hii kufungwa magoli 7 kwa 1 na Ujerumani katika hatua ya nusu fainali huo ukiwa ni mchezo wa kwanza Brazil kupoteza nyumbani baada ya miaka 39 kupita.

                         Scolari akitoa maelekezo kwa Marcelo.

Matokeo ya usiku wa kuamkia leo ya kufungwa michezo miwili mfululizo yamefikia rekodi ya mwaka 1940  ambapo Brazil ilipoteza michezo miwili mfululizo kwenye ardhi ya nyumbani.

Katika fainali za mwaka huu za kombe la dunia Brazil imeshinda michezo mitatu,kufungwa miwili na kutoka sare mara mbili nakisha kushinda kwa mikwaju ya penalty dhifi ya Chile.

                           Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment