Na Boniface Wambura, DAR
ES SALAAM.
SEMINA na mtihani wa utimamu wa mwili (physical fitness test) kwa waamuzi wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na baadhi ya wale wa daraja la kwanza wenye kiwango cha juu (elite) itafanyika jijini Dar es Salaam.
Waamuzi 30 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar watashiriki kwenye semina hiyo itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia Julai 21 hadi 26 mwaka huu.
Mkufunzi wa FIFA kwa Kanda ya Kusini mwa Afrika, Carlos Henriques kutoka Afrika Kusini ndiye atakayeendesha semina hiyo akisaidiwa na Watanzania Charles Mchau kutoka Kilimanjaro, Juma Ali David (Zanzibar), Joan Minja (Dar es Salaam) na Riziki Majala (Pwani).
Kwa upande wa waamuzi wa daraja la kwanza
ni Abdallah Kambuzi (Shinyanga), Agnes Pandaleo (Arusha), Ahamada Simba
(Kagera), Arnold Bugado (Singida), Charles Simon (Dodoma), Dalila Jafari
(Zanzibar), Frank Komba (Pwani), Helen Mduma (Dar es Salaam), Issa Bilali
(Zanzibar) na Issa Haji (Zanzibar).
Wengine ni Janeth Balama (Iringa), Jonesia Rukyaa (Kagera), Lulu Mushi (Dar es Salaam), Martin Saanya (Morogoro), Mary Kapinga (Ruvuma), Mbaraka Haule (Zanzibar), Mfaume Ally (Zanzibar), Mohamed Mkono (Tanga) na Soud Lila (Dar es Salaam).
Washiriki wa semina hiyo na wakufunzi wanatakiwa kuwasili jijini Dar es Salaam, Julai 20 mwaka huu.
Wengine ni Janeth Balama (Iringa), Jonesia Rukyaa (Kagera), Lulu Mushi (Dar es Salaam), Martin Saanya (Morogoro), Mary Kapinga (Ruvuma), Mbaraka Haule (Zanzibar), Mfaume Ally (Zanzibar), Mohamed Mkono (Tanga) na Soud Lila (Dar es Salaam).
Washiriki wa semina hiyo na wakufunzi wanatakiwa kuwasili jijini Dar es Salaam, Julai 20 mwaka huu.
Kikosi cha Serengeti boys
Wakati huo huo: Waamuzi wa mechi ya
kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya
miaka 17 kati ya Tanzania (Serengeti Boys) na Afrika Kusini (Amajimbos)
wanawasili leo (Julai 15 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Mechi hiyo itafanyika Ijumaa (Julai 18 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam na itachezeshwa na waamuzi hao kutoka Shelisheli. Kiingilio cha mechi hiyo ni sh. 2,000 tu.
Waamuzi hao ambao wanawasili saa 2.05 usiku kwa ndege ya Kenya Airways ni Allister Barra, Gerard Pool, Jean Joseph Felix Ernest na Nelson Emile Fred.
Kamishna wa mechi hiyo Andriamiasasoa Doda Nirimboavonjy kutoka Madagascar pia anawasili leo saa 2.05 usiku kwa ndege ya Kenya Airways.
Mkule.blogsport.com
No comments:
Post a Comment