Pages

Ads 468x60px

Monday, July 28, 2014

PIGO MAN UNITED RAFAEL AUMIA ZIARANI NCHINI MAREKANI.




                                                          Rafael Da Silva.

Mlinzi wa klabu ya Manchester United, Rafael Da silva amerejea nchini Uingereza kwa ajili ya matibabu kutokana na kuumia nyonga akiwa ziarani nchini Marekani. 

Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil aliumia wakati wa mazoezi jijini Denver kuelekea katika mchezo wa kirafiki walioshinda magoli  matatu kwa mawili dhidi ya AS Roma.

Rafael kuna uwezekano asicheze tena michezo ya kujipima nguvu kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu England inayotarajiwa kuanza mwezi ujao huku  kurejea kwake nyumbani kunampa matumaini ya kupona haraka.

Manchester United itafungua pazia la Ligi Kuu England mwezi ujao kwa kucheza na Swansea City katika Uwanja wa Old Trafford Agosti 16 mwaka huu.
                             
                     Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment