Pages

Ads 468x60px

Tuesday, July 15, 2014

ANTONIO CONTE ABWAGA MANYANGA NDANI YA JUVE.



                             Antonio Conte.

Kocha wa mabingwa wa ligi kuu ya Italia maarufu kama Serie A wa klabu ya Juventus , Antonio Conte ametangaza kujiuzulu nafasi yake.
Conte  mwenye umri wa miaka arobaini na nne ameachia ngazi kuifundisha timu hiyo akiwa amebakiza mwaka mmoja mkataba wake kumalizika.
Mabingwa hao wa italia wamethibitisha kujiuzulu kwa kocha huyo kupitia tovuti yao huku wakieleza kuwa wamesikitishwa na uamuzi huo ambao umekuwa wa ghafla kwao lakini hata hivyo wamekubali ombi hilo.
Hata hivyo Conte amewashukuru wachezaji wa kikosi hicho kwa mchango waliompa katika kipindi chote alichokuwepo kwenye klabu hiyo huku akiwataka kujiandaa vizuri kwa msimu unaokuja ili kutetea ubingwa wao.


                Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment