Pages

Ads 468x60px

Wednesday, July 16, 2014

KAZI IMEANZA KUJIANDAA NA MSIMU MPYA WA BPL OLD TRAFORD.



                               Louis Van Gaal.

Kocha mpya wa timu ya Manchester United Louis Van Gaal amewasili leo mjini Manchester tayari kwakuanza kazi ya kuwanoa mabingwa wao mara 20 wa ligi kuu ya England.

Akiwa katika siku yake ya kwanza Van Gaal mwenye umri wa miaka 62 amewasili kwenye uwanja wa mazoezi wa Carrington ambao unatumiwa na Manchester United.

Van Gaal ambaye ameisaidia Uholanzi kushika nafasi ya tatu kwenye kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil  mchezo wake wa kwanza akiwa kocha wa Man United utakuwa dhidi ya Valencia tarehe 12 ya mwezi ujao hili likiwa pambano la kirafiki.

Kocha huyo kibarua chake cha kwanza katika ligi kuu ya England ataikabili Swansea City tarehe 16 ya mwezi ujao na baada ya Man United kufanya usajili wa Luke Show na Herrera timu hiyo inawawinda Angel Di Maria na kiungo  Arturo Vidal wa Juventus.

                     Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment