Pages

Ads 468x60px

Wednesday, July 16, 2014

HUYU NDIYE MRITHI WA CONTE NDANI YA JUVENTUS.



                                 Massimiliano  Allegri


Mabingwa  wa ligi kuu ya Italia Juventus  wanataraji kumteua kocha wa zamani wa  AC Milan Massimiliano  Allegri kuchukua nafasi ya Antonio Conte aliyejiuzulu  hapo jana.

Imeelezwa kuwa Allegri amefikia makubaliano na uongozi wa Juventus wa kuifundisha timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili na uteuzi huo unataraji kutangazwa rasmi wakati wowote kutoka sasa.
Uongozi wa Juve chini ya rais wake Andrea Agnelli asubuhi ya leo jumatano umfanya mazungumzo na Allegri nafikia makubaliano ya kumpa kocha huyo mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya Euro milioni 2 kwa msimu pamoja na bonasi mbalimbali.

Allegri ambaye amekuwa hana kazi tangu atimuliwe na AC Milan mwezi wa kwanza mwaka huu anatarajiwa kuanza kazi kesho alhamisi 

                         Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment