Pages

Ads 468x60px

Thursday, July 31, 2014

NADAL KUKAA NJE WIKI MBILI HADI TATU.





                                        Rafael Nadal.

Mcheza Tenisi Rafael Nadal anataraji kukaa nje ya uwanja kwa majuma matatu baada ya kuuumia  kifundo cha kiganja wakati akifanya mazoezi  jumanne ya wiki hii.

Kuumia kwa mchezaji huyo anayeshika nafasi ya pili kwa ubora wa Tenisi duniani kumekuja ikiwa ni majuma kadhaa  kabla ya kuanza kwa mashindano ya wazi ya marekani yanayotaraji kufanyika mjini New York Marekani.

Nadal mwenye umri wa miaka 28 kwasasa atashindwa kutetea mataji yake ya michuano ya Toronto  na Cincinnati mwaka huu huku ikielezwa atakuwa tayari kurejea uwanjani kwenye michuano ya wazi ya Marekani inayoanza  tarehe 25 ya mwezi wa nane.

Mchezaji huyo amethibitisha kuwa ameumia kifundo cha mkono wake wa kulia wakati akiwa mazoezini na anataraji kupatiwa matibabu   na madaktari wake yatakayomfanya atumie majuma mawili hadi matatu ili kupona.

                     Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment