Pages

Ads 468x60px

Tuesday, July 22, 2014

BALAA NYOTA MPYA WA JUVENTUS AUMIA MAZOEZINI KUKAA NJE YA SIKU 50





             Alvaro Morata akikabidhiwa jezi yake ndani ya Juve.

Kiungo mpya wa Juventus ya Italia Alvaro Morata aneanza vibaya maisha yake mapya  na timu hiyo baada ya kuelezwa anataraji kukaa nje ya uwanja wa muda wa siku 50 kutokana na jeraha na goti.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 ambaye alijiunga na Juve jumamosi iliyopita  ameumia akiwa mazoezini katika simu yake ya kwanza na mabingwa hao wa ligi kuu ya Italia Serie A.

Morata  ambaye alijiunga na Juve akitokea Real Madrid kwa dau la Euro milioni 20 ililazimika kutolewa nje baada ya kuumia goti la kushoto  kisha kukimbizwa kwenye hospitali mjini Turin kisha kufanyiwa vipimo.

Raia huyo wa Hispania ni mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Monaco msimu huu chini ya kocha mpya Massimiliano Allegri na mara baada ya kupona atapaswa kuchuana vikali na wachezaji Carlos Teves,na Fernando Llorente kuanza kwenye kikosi cha kwanza.

                                      Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment