Pages

Ads 468x60px

Friday, July 25, 2014

TUTAENDELEZA VITA VYA USAJILI ASEMA PEREZ.





                           Rais wa Real Madrid  Florentino Perez.


Baada ya kuwasajili nyota wawili wapya katika msimu huu wa usajili barani Ulaya rais wa Real Madrid Florentino Perez amesema klabu hiyo itaendeleza mawindo yake hadi siku ya mwisho ambapo dirisha la usajili litafungwa.

Perez amesema hata siku ya mwisho kabla ya kufungwa kwa dirisha wanaweza kusajili au kufanya mauzo ya mchezaji huku akisistiza kwamba wanataka kuiimarisha timu yao hivyo uwezekano wa kuongeza wachezaji upo hadi mwisho wa mwezi ujao.

Mabingwa wao wa Ulaya kwa upande wa vilabu tayari wamesha wasajili wachezaji Toni Kroos kutoka Bayern Munich na mshambuliaji Jemes Rodriguez kutoka Monaco huku usajili wa mlindamlango wa Levante Keylor Navas unatarajiwa wakati wowote.

Real Madrid itacheza na Atletico Madrid tarehe 19 ya mwezi wa 8  na kurudiana tarehe 22 mwezi huohuo katika mchezo wa ngao ya jamii kuashiria kuanza msimu mpya wa La Liga 2014/2015.

                              Peres akiwa na Luis Figo.

                                    Perez na C.Ronaldo.

                                             Perez na G.Bale.

                            Perez akiwa na Toni Kroos.

                            Perez akiwa na Jemes Rodriguez.
                   
                                Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment