Jaja alipopokelewa leo uwanja wa ndege wa Jk Nyerere.
Mshambuliaji wa kimataifa
kutoka nchini Brazil Geilson Santos Santana "Jaja" amewasili leo
mchana jijini Dar es salaam akitokea jijini Sao Paul tayari kwa kuanza kazi ya
kuitumikia klabu ya Young Africans Sports Club kwa msimu wa 2014/2015.
Jaja ambaye alikua
akichezea timu ya Itabaina FC nchini Brazil, anakuwa ni mchezaji wa pili
kuungana na kikosi cha Young Africans baada ya Andrey Coutinho kuwa mchezaji wa
kwanza kujiunga na kikosi cha kocha Marcio Maximo.
Usajili wa wachezaji hawa
ni muendelezo wa uongozi wa Young Africans kuhakikisha msimu ujao unakua na
kikosi bora ambacho kitaweza kufanya vizuri kwenye michuano ya Ligi Kuu ya
Vodacom na mashindano ya Kombe la Shrikisho Barani Afrika.
Jaja anaungana na makocha
wabrazil Marcio Maximo na Leonardo Neiva na kiungo Andrey Coutinho katikaa
msimu huu ambapo kwa pamoja ushirikiano wao na wachezaji wengine wazawa
wataisaidia Young Africans kufanya vizuri.
Kesho asubuhi Jaja
anatarajiwa kuanza mazoezi katika shule ya sekondari Loyola ikiwa ni sehemu ya
maandaliz ya michuano mbalimbali itayowakabili.
Mkule.blogsport.com
No comments:
Post a Comment