Pages

Ads 468x60px

Tuesday, July 29, 2014

BISHOO RONALDINHO AVUNJA MKATABA WAKE NA ATLETICO MINEIRO.





                                                              Ronaldinho Gaucho

Kocha mkuu wa timu ya Atletico Mineiro ya nchini Brazil Levir Culpi amethibitisha kuwa wamevunja mkataba na mshambuliaji  mkongwe wa kikosi hicho Ronaldinho Gaucho ambaye amewahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia.
Ronadinho ambaye alisaini mkataba mpya wa mwaka mmoja mwezi wa kwanza mwaka huu licha ya kwamba alikuwa na nia ya kuhamia timu ya Besiktas ya Uturuki.
Kocha wa Mineiro mbali na kumshukuru nyota huyo wa zamani wa Fc Barcelona na timu ya taifa ya Brazil kesho jumatano Ronaldinho anatarajiwa kuwa na mkutano na waandishi wa habari kutangaza matarajio yake ya baadae.
Ronaldinho ambae  alijiunga na Atletico Mineiro mwezi wa sita mwaka 2012 baada ya kuachana na timu ya Flamengo licha ya kuhusishwa na mipanggo ya kujiunga na Boca Junior inayosaka mrithi wa Juan Roman Riquelme pia inaelezwa huenda akajiunga na ligi ya Marekani MLS.
                   Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment