Pages

Ads 468x60px

Thursday, July 24, 2014

SANTOS YAHOFIA MKWANJA KUMSAJILI ROBINHO.





                                       Robinho.

Makamu wa rais wa klabu ya Santos nchini Brazil Odilio Rodrigues amesema timu hiyo itapenda kumsajili mshabuliaji wa AC Milan ya Italia Robinho kama mchezaji huyo atakubaliana nao juu ya masuala ya malipo.

Robinho ambaye yupo kwenye timu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya Brazil kwa mkopo tangu msimu uliopita  amewahi kushinda mataji mawili ya ligi kabla ya kuhamia Real Madrid mwaka 2005.

Kiongozi huyo wa juu wa Santos amesema wameshafanya mawasiliano na mwanasheria wa mchezaji huyo ili kuona kama atakubali kubakia nao lakini suala la malipo kwa nyota huyo huenda ikawa sababu ya kutofanikisha usajili wake.

Baada ya kuitumikia Real Madrid kwa miaka mitatu Robinho alitumia miaka miwili akiwa na Manchester City ya England kabla ya kujiunga na Milan mwaka 2010 na kufunga magoli 32 akiwa San siro.

                                 Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment