Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM.
WASHAMBULIAJI Thomas Ulimwengu na Mbwana Samata wa klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wanawasili nchini keshokutwa alfajiri (Julai 16 mwaka huu) kwa ajili ya mechi dhidi ya Msumbiji (Mambas).
Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika (AFCON) kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Mambas itachezwa Jumapili (Julai 20 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro
Premium Lager imepiga kambi Tukuyu mkoani Mbeya ikijiandaa kwa mechi hiyo
itakayochezeshwa na mwamuzi Mahmoud Ashour kutoka Misri.
Stars itarejea jijini Dar es Salaam siku ya Ijumaa (Julai 18 mwaka huu) kwa ajili ya mechi hiyo wakati Mambas nao wanatarajiwa kutua siku hiyo hiyo. Mechi ya marudiano itachezwa kati ya Agosti 1 na 3 mwaka huu nchini Msumbiji.
Mkule.blogsport.com
No comments:
Post a Comment