Kikosi cha timu ya taifa ya Cape Verde.
Cape verde
ni taifa lililopata uhuru wake kutoka kwa Ureno mwaka 1975.
Hiki ni
kisiwa kidogo kilichopo katika bahari ya Atlantic chenye watu wapatao 498 897 (laki nne tisini na nane elfu,mia
nane na tisini na saba).kwa takwimu za mwaka 2013.
Mji wake
mkuu ni Praia .
Miongoni mwa
miji mashuhuri katika taifa hili ni..Boa Vista,santa maria Cape verde mji
mashuhuri kwa uvuvi wa samaki uliopo km 16 kutoka kusini mwa uwanja wa ndege wa
Amílcar Cabral, miji miningine ni kama Pedra Lume salt crater, Olho Azul, Buracona na Fontana.
Lugha kuu ya
raia wa taifa hili ni Kireno.
Rais wa nchi
hii ni ... Jorge
Carlos de Almeida Fonseca aliyeingia madarakani sept 9 mwaka
2011 akichukua nafasi ya Pedro Verona Rodriguez Pires aliekaa madarakani kuanzia march 22 mwaka
2001 hadi sept 9 mwaka 2011.
Tangu ipate
uhuru wake kutoka kwa Wareno mwaka 1975 nchi hii imeongozwa na marais wanne tuu
ambao ni Aristides Maria Pereira julai 8 1975 hadi januari
1981,januari 1981 hasi march 22 mwaka 1991 na kumpisha António Mascarenhas Monteiro, kuanzia 22 March 1991 hadi
22 March 2001 kisha Pedro Verona Rodrigues Pires kupewa kijiti cha urais kuanzia 22 March 2001
hadi 9 September 2011 naye kumpa kijiti
hicho cha urais Jorge
Carlos de Almeida Fonseca kuanzia 9 September 2011 ambaye yupo madarakani hadi hivi sasa.
Timu ya soka
ya taifa ya Cape verde inajulikana kwa jina la utani kama Blue Sharks yaani Papa
buluu.wakijivunia samaki huyo anayepatikana kwa wingi katika bahari ya
Atlantic.
Ni samaki mkubwa
ambaye hupatikana katika bahari kubwa duniani na inaelezwa hufikia uzito mkubwa
kabisa wa kg 391.
Cape verde
inashika nafasi ya 40 katika ubora wa soka duniani katika takwimu zilizotolewa
januari 18 mwaka huuwa 2015.
Nafasi ya
juu kabisa iliyoshika nchi hii katika ubora wa soka duniani ni ya 27 na hii
ilikuwa february mwaka 2014 huku nafasi
ya chini kabisha kushikwa na taifa hilo ni ya 182 ilikuwa ni April mwaka 2000.
Kwamara ya
kwanza Cape Verde kucheza mechi ya kimataifa ilikuwa mwaka 1978 ambapo hatahivyo
tarehe na mwezi havikuwekwa wazi
walicheza na Angola na kufungwa goli 1 kwa 0.
Ushindi
mkubwa iliyowahi kuupata Cape verde ni wa magoli 5 kwa 0 dhidi ya Equetorial
Guinea march 28 mwaka 2009 na kipigo kikubwa walichowahi kukipata ni cha magoli
5 kwa 1 dhidi ya Senegal february 12 1981.
Pia vipigo
vikubwa waliowahi kuvipata ni magoli 4 kwa 0 kutoka kwa Ghana Octoba 8 mwaka 2005 pamoja na kipigo
kama hicho walichokipata kutoka kwa Guinea september 9 mwaka 2007.
FAINALI ZA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA
(AFCON).
Mashabiki wa soka nchini Cape Verde hawapo mbali na timu yao,hapa walikuwa nayo nchini Afrika kusini 2013.
Mashabiki wa Cape Verde wakifanya yao nchini Afrika kusini katika fainali zilizopita ambapo timu yao ya taifa iliishishia robo fainali.
Mara ya
kwanza kwa Cape verde kushiriki fainali hizi ni mwaka 2013 ambapo ilifanikiwa
kutinga hatua ya robo fainali fainali
zilizofanyika nchini Afrika ya kusini na Nigeria kutawazwa mabingwa baada ya
kuifunga Burkinafaso goli 1 kwa 0.
Kinara wa magoli
kwenye timu ya taifa ya Cape verde ni mchezaji Carlos Morais, Héldon Ramos mwenye magoli 10.
Kocha mkuu
wa timu hiyo hivi sasa ni Rui
Águas kwakirefu jina
lake ni Jose Rui Lopes Aguas mzaliwa wa Lisbon Ureno na nyota wa zamani wa
Benifica ya Ureno.
Nahodha wa
timu hii ni Marco Soares anyecheza
nafasi ya kiungo akiichezea pia klabu ya AC Omonia ya nchini Cyprus.
Katika fainali za mwaka huu zinazofanyika nchini Guinea Cape Verde
imepangwa kwenye kundi B lenye mataifa ya ZAMBIA,TUNISIA,na DR CONGO.
Je taifa hili changa kisoka litaendelea kuuteka umma wa Afrika kwenye
fainali za mwaka huu wakiwa wanashiriki kwa mara ya pili?wapo wasio lipa nafasi
taifa hili linalokua kwa kasi kisoka licha ya kutosheheni majina makubwa
umaarufu kwao sio tija bali wanajivunia vipaji lukuki walivyobarikiwa Kama ...viungo
Toni Varela,Nuno Rocha,Garry Rodriguez na Monteiro Masedo ambaye ni fundi wa kupiga mipira kwa
miguu yote huku safu ya ushambuliaji ikiongozwa na wakali kama ...Ryan Mendez, Jorge Djaniny na Julio Tavares ambaye uzito wake wa kg 85
haumsumbui kufanya chochote kwenye lango la adui.
Hawa ndio Cape Verde wenyeyewe
wanajiita( Blue
Sharks)yaani PAPA BLU.
Naamini
mashabiki wa Cape verde kama ndugu yangu Luther Akyoo mtakuwa mmefarijika kwa
historia fupi ya taifa hili changa kisoka lakini ni moto wa kuotea mbali.
Mkule.blogsport.com
No comments:
Post a Comment