Pages

Ads 468x60px

Friday, July 18, 2014

JESHI LA VAN GAAL LITAKALOANZA STYLE ZA KIDACHI HILI HAPA.



          Kocha wa nachester United Louis Van Gaal

Kocha mkuu wa mancheter United Louis Van Gaal Ametangaza orodha ya wachezaji wapatao 25 watakaosafiri na kikosi hicho kuelekea Marekani kucheza mechi za kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu ya England unaotaraji kuanza mwezi ujao.

Katika orodha hiyo wapo nyota 10 walioshiriki kwenye fainali za kombe la dunia nchini Brazil kwakuziwakiliza timu zao za taifa wakiongozwa na Wayne Rooney pamoja na wachezaji wapya Luke Show na Ander Herrera.

wachezaji waliokuwepo kwenye kombe la dunia mwaka huu wakiwa kwenye vikosi vya timu zao za taifa ni  Luke Shaw, David de Gea, Shinji Kagawa, Chris Smalling, Phil Jones, Juan Mata, Antonio Valencia, Danny Welbeck na Luis  Nani.

wachezaji ambao hajajumuishwa kwenye safari hiyo ya kwenda Marekani kwa sababu ya timu zao za taifa kuingia hatua raundi ya pili  ni Patrice Evra, Javier Hernandez, Robin van Persie, Adnan Januzaj na  Marouane Fellaini.
Van Gaal pia amewajumuisha chipkizi Tyler Blackett  na  Jesse Lingard  ambao wamepewa nafasi  kutokana na kuwa na dalili za  kumvutia kocha huyo.
 
Ikiwa Marekani United itacheza  mchezo wa kwanza wa  kirafiki na LA Galaxy  july 23 kabla ya kucheza michezo mingine na Roma,Inter Milan na Real Madrid kati ya july 26,juky 29 na Augost 2 mwaka huu.



Hiki ni kikosi kamili cha Manchester United kitakachoanza ziara yake nchini Marekani: David de Gea, Anders Lindegaard, Sam Johnstone, Ben Amos, Rafael, Jonny Evans, Chris Smalling, Phil Jones, Luke Shaw, Tyler Blackett, Michael Keane, Reece James, Ander Herrera, Tom Cleverley, Darren Fletcher, Ashley Young, Wilfried Zaha, Shinji Kagawa, Juan Mata, Antonio Valencia, Nani, Jesse Lingard, Danny Welbeck, Will Keane, Wayne Rooney.

                                  Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment