Pages

Ads 468x60px

Friday, July 25, 2014

RHYS AFUNGIWA KUSHIRIKI MICHUANO YA JUMUIYA YA MADOLA MJINI GLASGOR.




                                            Rhys Williams.

Mwanariadha Rhys Williams raia wa Wales  ameondolewa kushiriki mashindano ya jumuiya ya madola inayoendelea mjini Glasgow nchini Scotland baada ya kushindwa kufaulu vipimo vya afya alivyofanyiwa julai 11 mwaka huu.

Nahodha huyo wa timu ya riadha ya Wales alifanyiwa majaribio ya vipimo kubaini kama anatumia dawa za kuongeza nguvu na matokeo ya vipimo hivyo yamebaini kuwa mwanariadha huyo alikutwa na hatia.

Williams ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Ragby wa Wales JJ Williams baada ya kubainika kutumia dawa za kuongeza nguvu amepigwa marufuku kushiriki mashindano yote  yanayoandaliwa  Uingereza.

Tovuti ya timu ya riadha ya Wales imethibitisha kupokea adhabu hiyo na kusema wamekubaliana na uamuzi uliochukuliwa dhidi ya mwanariadha huyo.

                                              Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment