Pages

Ads 468x60px

Friday, January 16, 2015

NYOTA WA ZAMANI WA UFARANSA ATANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS WA FIFA.



                                       David Ginola.

Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya ufaransa David Ginola ametangaza nia ya kugombea kiti cha uraisi kwenye shirikisho la soka duniani FIFA akipambana na raisi wa sasa sepp blatter katika uchaguzi unaotaraji kufanyika baadae mwaka huu.

Nyota huyo alikua balozi wa uingereza wakati ikiwania kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia 2018 ameomba kuungwa mkono na shirikisho la soka barani ulaya na vyama vitano vya mashirikisho ya soka.

Ginola ambaye alivichezea vilabu vya Newcastle utd,tottenham hotspurs na everton  mwaka 2002,anataraji kukutana na waandishi wa habari leo jijini London.

Wakati huohuo makamu wa raisi wa fifa Ali Bin Al Hussein,pamoja na Jerome champagne ambao kwa pamoja walijiunga na FIFA mwaka 1999,wanataraji kutangaza kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho.
Blatter amekuwa raisi wa FIFA tangu mwaka 1998 na sasa anawania kugombea kwa msimu wa tano lakini wagombea kadhaa wamejitokeza kupambana nae kwenye uchaguzi ujao.
      
                                   Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment