Kikosi cha yanga kikiwa mazoezini kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara unaotaraji kuanza sept 20 2014.
Timu ya
Young Africans kesho itashuka kwenye dimba la Uwanja wa Taifa kupambana na timu
ya Thika United inayoshiriki Ligi Kuu nchini Kenya katika mchezo wa kirafiki wa
Kimataifa wa kujipima nguvu kabla ya kuanza kwa mikikimikiki ya Ligi Kuu ya
Vodacom Septemba 20 mwaka huu.
Mchezo wa
kesho unatarajiwa kuwa kipimo kizuri kwa kikosi cha mbrazil Marcio Maximo
ambacho kimeshacheza michezo mitatu mpaka sasa ya kirafiki dhidi ya timu za
Chipukizi FC, Shangani FC na KMKM zote za Ligi Kuu ya Zanzibara na kuibuka na
ushindi kwa michezo yote.
Young
Africans ambayo ina kikosi cha wachezaji 31 wakiwemo vijana sita kutoka kikosi
cha cha U20 waliopandishwa itacheza mchezo wake wa kwanza wa kimataifa chini ya
kocha mkuu Marcio Maximo na msaidizi wake Leonardo Neiva ambao wote ni raia wa
Brazil.
Mechi
itarajiwa kucheza kuanzia majira ya saa 11:00 jioni kwa saaa za Afrika
Mashariki ili kutoa fursa kwa wafanyakazi wa maofisini, taasisi mbalimbali
waweze kuwahi na kushuhudia mchezo huo.
Viingilio
vya mchezo huo ni:
VIP A Tshs
30,000/=
VIP B &
C Tshs 20,000/=
Orange Tshs
10,000/=
Bluu &
Kijanni Tshs 5,000/=
Tiketi
zitaanza kuuzwa kesho saa 3:00 asubuhi katika eneo la Uwanja wa Taifa.
Wanachama,
wapenzi washabiki na wadau wa soka kwa ujumla mnaombwa kujitokeza kwa
wing kesho kwenye dimba la Uwanja wa Taifa kuja kuwashangilia vijana
wakipeperusha bendera ya kijani na njano kutoka mitaa ya Twiga/Jangwani.
Mkule.blogsport.com
No comments:
Post a Comment