Pages

Ads 468x60px

Friday, September 5, 2014

VIDAL KUIKACHA KAMBI YA TIMU YA TAIFA YA CHILE KWA JERAHA LA GOTI.



                                      Arturo Vidal

Kiungo wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Chile anataraji kuukosa mchezo ujao wa kirafiki baina ya  timu yake ya taifa na Haiti unaotaraji kuchezwa tarehe 10 ya mwezi huu kutokana na kuwa majeruhi.
Vidal mwenye umri wa miaka 27 imeelezwa kuwa anasumbuliwa na maumivu ya goti  alililofanyiwa upasuaji kabla ya kuanza kwa fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil ambapo Chile ilifanikiwa kuingia hatua ya 16 bora.
Rais wa shirikisho la soka nchini Chile  Sergio Jadue  amethibitisha mchezaji huyo  kutokuwa kwenye hali nzuri hivyo  ataondoka  kwenye kambi ya timu ya taifa   mara baada ya mchezo wa leo wa kirafiki dhidi ya  Mexico..
Rais huyo amesema  wakati Arturo Vidal akiondoka kwenye kambi ya timu ya taifa mara baada ya mchezo huo wa leo wa kirafiki wachezaji wengine wataendelea  kubaki kambini hapo kwa maandalizi zaidi ya pambano lao na Haiti.

                             Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment