Pages

Ads 468x60px

Wednesday, September 3, 2014

BEN FOSTER AENGULIWA KATIKA KIKOSI CHA ENGLAND KINACHOIVAA NORWAY LEO.



                                               Ben Foster.

 Mlinda mlango wa timu ya taifa ya Uingereza Ben Foster ameenguliwa katika hicho kianachojiandaa kucheza mchezo wa kirafiki leo dhidi ya Norway baada ya kuumia akiwa mzoezini.
Chama cha soka nchini Uingereza  FA kimethibitisha kuwa mbali na kuukosa mchezo huo wa leo utakaochezwa kwenye uwanja wa Wembley pia hatosafiri na  kikosi cha timu ya taifa kitakachocheza na Uswis juma lijalo kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Ulaya 2016.
FA imesema kocha mkuu Roy Hodgson  hatoita mlinda mlango  mwengine na badala yake mlinda mlango nambari moja Joe Hart ataendelea  na jukumu hilo licha na yeye  kusumbuliwa na maumivu ya kidole gumba cha mkono.
Kikosi hicho cha Uingereza  leo kitakuwa kikiongozwa na nahodha mpya  Wayne Rooney ambaye aliteuliwa  hivi karibuni kuchukua nafasi ya Steven Gerard aliyestaafu kuichezea timu ya taifa.

                                       Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment