Pages

Ads 468x60px

Monday, September 8, 2014

SOMA ALICHOKISEMA MORINHO JUU YA VAN GAAL.



 Lois Van Gaal akikabidhiwa jezi alipokuwa akitambulishwa kuwa kocha mpya wa Manchester United.


Wakati ligi kuu ya Uingereza ikitaraji kuendelea mwishoni mwa juma hili kocha mkuu wa Chelsea Jose Mourinho amesema anamatumaini  Manchester United  itaimarika chini ya kocha mpya Lois Van Gaal licha ya kuanza vibaya.
Mourinho ambaye aliwahi kufanya kazi chini ya Van Gaal katika klabu ya Fc Barcelona  amebainisha kuwa hana hofu na uwezo wa kocha huyo na kwamba ni mtu mwenye uzoefu mkubwa hivyo anafaa kuinoa Manchester United.
Mourinho amesema United ni klabu kubwa duniani na Van Gaal ni kocha mkubwa ambaye anamkubali kwa muda mrefu  na licha ya kuanza vibaya katika ligi anaweza kuutumia ukongwe wake katika kazi kuipa mafanikio timu hiyo ya jijini Manchester.
Akizungumzia kikosi chake cha Chelsea Mourinho ambaye ni raia wa Ureno amebainisha kuwa timu yake ni imara na  inawachezaji wa aina tofauti  na wazuri zaidi ya msimu uliopita hivyo anamatumaini ya kutwaa ubingwa msimu huu.

                              Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment