Pages

Ads 468x60px

Tuesday, September 16, 2014

HEATHER WATSON ACHEZEA KICHAPO KATIKA MICHUANO YA WAZI YA KOREA.



                                Heather Watson.

Mwanadada wa Kiingereza Heather Watson ameiaga mapema michuano ya wazi ya Korea katika Tenisi baada ya kufungwa kwenye  mzunguko wa kwanza na Nicole Gibbs mpambano uliochezwa leo.
Watson mwenye umri wa miaka 22 ambaye anashika nafasi ya 46 kwa ubora wa Tenisi duniani kwa wanawake amepoteza mchezo huo kwakufungwa seti 7 kwa 5,na 6 kwa 2  na mpinzani wake Nicole Gibbs anayeshika nafasi 101 kwa ubora duniani.
Mwezi uliopita Heather Watson aliondoshwa katika mzunguko wa kwanza na mwanadada Sorana Cirstea wa Romania kwenye michuano ya wazi ya Marekan kwa seti 6 kwa 1 na 6 kwa 1 pambano lilodumu kwa dakika 54.

                               Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment