Pages

Ads 468x60px

Wednesday, September 3, 2014

KOMPANY HATARINI KUKOSA PAMBANO LA LEO KATI YA UBELGIJI NA AUSTRALIA.



                                             Vicent Kompan.

Nahodha wa timu ya taifa ya Ubelgiji na klabu ya Manchester City Vicent  Kompan anataraji kufanyiwa  vipimo vya nyama za paja  baada ya kuumia akiwa mazoezini leo na kikosi chake cha timu ya taifa.
Kocha mkuu wa Ubelgiji  Marc Wilmots mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 28 amewahishwa hospitali kwa uchunguzi zaidi  na yupo kwenye hatihati ya kukosa  pambano  la leo la kirafiki dhidi ya Australia.
Kocha huyo amesema nahodha huyo aliyesajiliwa na Man City mwaka 2008 akitokea Hambarg  anauwezekano mkubwa wa kulikosa pambano hilo kama atakuwa ameumia sana ili kumuepusha na maumivu makali zaidi.
Kompan ambaye amekuwa mhimili mkubwa katika  nafasi ya ulinzi ya mabingwa wa ligi kuu ya England Manchester City  kiasi cha kuisaidia kutwaa ubingwa   wa ligi mara mbili msimu wa 2011/2012 pamoja na msimu wa 2013/2014.

                                Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment