Miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara Azam fc.
AZAM FC inaingia kambini leo katika
hosteli za Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, kujiadaa na mechi ya Ngao ya
Jamii dhidi ya Yanga SC Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Meneja wa Azam FC, Jemadari Said
Kazumari amesema timu itaingia kambini jioni ya leo katika hosteli za Azam
Complex, Chamazi, Dar es Salaam kuelekea mchezo huo wa Ngao ya Jamii.
Amesema wachezaji wawili beki Wazuri
Salum na mshambuliaji, John Bocco ni majeruhi na hawamo kwenye program za
mchezo huo.
“Tuna majeruhi wawili ambao
hawatakuwepo kwenye programu ya mchezo wa Ngao ya Jamii, ambao ni beki Waziri
Salum na Nahodha wetu, John Bocco,”amesema mshambuliaji huyo wa zamani wa Kariakoo
United ya Lindi.
Bocco aliuamia katika mchezo wa Robo
Fainali Kombe la Kagame dhidi ya El Merreikh ya Sudan ambao Azam FC ilitolewa
kwa penalti baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90.
Jemadari amesema kwamba, wachezaji
wengine wote wapo fiti na wamekuwa wakiendelea na mazoezi Uwanja wa Azam
Complex na wanatarajiwa kuingia kambini leo.
Mabingwa hao wa Tanzania Bara
wanaonolewa na kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog watamenyana na washindi wa
pili, Yanga SC walio chini ya kocha Mbrazil, Marcio Maximo Jumapili Uwanja wa
Taifa.
Hii itakuwa mara ya tatu mfululizo,
Azam FC kucheza mechi ya Ngao ya Jamii na mara zote ikifungwa kwanza na Simba
SC na baadaye na Yanga SC- lakini safari hii kocha Omog anataka kupindua
matokeo hayo.
Mkule.blogsport.com
No comments:
Post a Comment