Pages

Ads 468x60px

Thursday, September 4, 2014

MOURINHO: NILITAKA TORRES AJIUNGE NA INTER MILAN NASIO AC MILAN.



                        Torres akiwa na kocha Jose Mourinho.

Kocha mkuu wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho amesema alimtaka mshambuliaji wa timu hiyo Fernando Torres kujiunga na Inter Milan badala ya AC Milan zote za nchini Italia katika msimu wa usajili uliomalizika hivi karibuni.
Mourinho ambaye ni raia wa Ureno amesema alitaka Torres ahamie Inter lakini hata kujiunga kwake na AC Milan ni uamuzi mzuri na ataweza kuisaidia vyema timu hiyo ambayo imekimbiwa na mshambuliaji Mario Balotelli aliyejiunga na Liverpool ya England.
Kocha huyo amesistiza kuwa mshambuliaji huyo anauwezo mzuri  hivyo kujiunga kwake na AC Milan kutampa fursa yakuonesha kipaji alichonacho ambacho kiliyumba tangu ajiunge na Chelsea kwa ada ya paund milioni 50 mwezi januari mwaka 2011 akitokea Liverpool.
Torres ambaye ni raia wa Hispania amejiunga na AC Milan kwa  mkopo wa  miaka miwili akitokea kwa matajiri wa jiji la Londond Chelsea siku chache kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

                                   Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment