Pages

Ads 468x60px

Monday, September 1, 2014

CAROLINE WOZNIACKI ATINGA ROBO FAINALI MICHUANO YA US OPEN.





                             Caroline wozniacki

Mchezaji Caroline Wozniacki amefuzu kuingia hatua ya robo fainali ya mashindano ya wazi ya Marekani kufuatia kupata ushindi dhidi ya mchezaji nambari tano kwenye mchezo wa tenesi duniani kwa upande wa wanawake Maria Sharapova.
Wozniacki anayeshikiria nafasi ya kumi kwenye mchezo huo duniani amepata ushindi dhidi ya Sharapova baada ya kufunga seti 6kwa4 , seti2kwa6, seti 6kwa2 licha ya mchezo kuwa wa upinzani mkali.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, amefuzu hatua hiyo ikiwa ni muda mrefu tangu mwaka 2012  ashiriki mashindano hayo na kuondoshwa katika hatua ya awali na kwa hivi sasa anajiandaa kukabili ana na Sara Errani kutoka Italia.
Sharapova ambaye amewahi kuwa bingwa wa zamani wa mashindano ya wazi ya Marekani  kwa mwaka 2011 ameungana na Simona Halep pamoja na Ana Ivanovic walioondoshwa mapema katika hatua ya awali ya mashindano hayo.

                                          Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment