Pages

Ads 468x60px

Sunday, September 14, 2014

SEMEONE ASIFU KIWANGO CHA TURAN ATLETICO IKIIADHIRI REALMADRID 2 KWA 1 SANTIAGO BERNABEU.



                           Kocha mkuu wa mabingwa wa La liga Atletico madrid Diego Semeone.

Kocha mkuu wa mabigwa wa ligi kuu ya Hispania Atletico Madrid Diego Semeone amemsifu mshambuliaj Arda Turan kwa uwezo mzuri aliouonyesha katika pambano la usiku wa jana dhidi ya Real Madrid ambapo timu yake ilishinda magoli 2 kwa1.
Mchezaji huyo ambaye aliingia  dakika ya 61 kuchukua nafasi Gabi  aliifungia Atletico Madrid goli la pili na la ushindi dakika ya 76  baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Juanfran  nakuifanya timu hiyo kuibuka na ushindi wa magoli hayo 2 kwa1.
Semeone ambaye ni raia wa Argentina  amesema katika mchezo huo timu yake ilicheza vyema kipindi cha kwanza lakini hakufurahishwa na  walivyoanza kipindi cha pili lakini alifurahishwa sana na kazi aliyoifanya Turan akitokea bench na kuwapaushindi.
Katika mchezo huo Atletico Madrid  ilijipatia magoli yake kupitia kwa Tiago na  Arda Turan  huku Real Madrid waliokuwa nyumbani Santiago Bernabeu kupata goli la kufutia machozi kupitia kwa mchezaji Cristiano Ronaldo.
  
                                     Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment