Pages

Ads 468x60px

Wednesday, September 10, 2014

FERRARI YAPATA PIGO MWENYEKITI WAKE AJIVUA GAMBA.



                                   Luca Di Montezemolo.


Mwenyekiti wa  Ferrari Luca Di Montezemolo ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo baada ya kuitumikia kwa muda wa miaka 23 timu ya Formula wani kufuatia matokeo mabaya waliyoyapata msimu huu.
Mwenyekiti huyo mwenye umri wa miaka 67 ameamua kuachia ngazi baada ya kutokubaliana na mkurugenzi mkuu Sergio Marchionne ambaye pia anafanya katika katika kampuni ya Fiat.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari mapema leo Di Montezemolo amesema amesikitishwa sana na ushiriki wa timu ya  Ferrari kwenye mashindano ya Formula wani hivyo hanabudi kuachia ngazi kumpisha mtu mwengine.
Katika taarifa yake Di Montezemolo aliyeshika nafasi ya uenyekiti wa Ferrari tangu mwaka 1991 amesema ni furaha na heshima kuwa kiongozi wa kampuni hiyo kubwa dunianilicha ya madereva wa timu hiyo kutoshinda mataji makubwa tangu mwaka 2008 pamoja na  ukongwe walionao.

      Luca Di Montezemolo akizungumza na waandishi wa habari leo kutangaza uamuzi wake wa kujiuzulu.
                         
                                     Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment