Pages

Ads 468x60px

Wednesday, September 10, 2014

NASSER AL KHATER: MAMBO YATAKUWA SAFI FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA 2022 NCHINI QATAR



                Mkurugenzi mtendaji  wa mawasiliano na mauzo wa Qatar Nasser Al Khater.

Wenyeji wa fainali za kombe la dunia mwaka 2022 nchi ya Qatar wanamatumaini makubwa kwa michuano hiyo kufanyika kwa amani licha ya changamoto ya haliya hewa kuendelea kutishia baadhi ya mafia hususani kutoka barani Ulaya.
Mkurugenzi mtendaji  wa mawasiliano na mauzo wa Qatar Nasser Al Khater amesema anaamini makubaliano ya michuano hiyo kufanyika majira ya joto au ya baridi yatafikiwa baina ya makundi mawili yanayopingana juu ya suala hilo.
 Khater amesema pamoja na nchi hiyo kukosolewa kwa kiasi kikubwa tangu kupewa uaandaaji wa fainali hizo wao wanaendelea na maandalizi na wameshaanza majaribio ya kufunga vifaa vya kukabiliana na joto katika viwanja hususani sehemu za kukaa mashabiki wa soka.
Pamoja na hayo yote kuendelea kiongozi huyo amesema upo uwezekano wa fainali hizo kufanyika kati ya januari na february mwaka 2022 au mwezi November na Desember au katika muda uliozoeleka ambao ni mwezi juni na julay  mwaka huohuo wa 2022.
                                 Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment