Pages

Ads 468x60px

Monday, September 15, 2014

ANCELOTTI: SINASHAKA NA KIBARUA CHANGU.



                                      Carlo Ancelotti.

Kocha mkuu wa klabu ya Real Madrid ya Hispania Carlo Ancelotti  amesema hana hofu yeyote  juu ya kibarua chake  licha  ya timu hiyo kupata matokeo mabaya hivi karibuni katika ligi kuu ya La Liga.
Ancelotti ambaye ni raia wa Italia amesema pamoja na sasa kuwa kwenye wakati mgumu  anaamini timu yake itaimarika kwakuwa inawachezaji wazuri  ambao wanauwezo wa kuleta matokeo mazuri siku za usoni.
Kocha huyo ambaye ataiongoza Real Madrid kesho kwenye  mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi klabu bingwa Ulaya dhidi ya Fc Basel amesema matumaini ya kutetea ubingwa wao wa Ulaya yapo pamoja na ushindani mkubwa  unaoonekana kuwepo msimu huu.
Kocha huyo wa zamani wa Chelsea amesema  zipo timu zimeimarika hususani Chelsea ya Uingereza  baada ya kusajili wachezaji kama Diego Costa, Cesc Fabregas, Filipe Luis na  ujio wa mlindamlango Thibaut Courtois umezidisha kasi ya klabu hiyo ya London.
                                     Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment