Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Utawala Bora wa klabu ya Young Africans Wakili Sam Mapande - kulia.
Uongozi wa klabu ya Yanga umesema
utapinga maamuzi ya kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji kuhusiana na
maamuzi yake ya kumtangaza mchezaji wake, Emmanuel Okwi kuwa huru.
Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria
ya Yanga, Sam Mapande amesema kuwa hawajaridhishwa na maamuzi hayo ambayo
yanakinzana na shitaka zima la mchezaji huyo.
Mapande amesema kuwa kamati ya TFF
imeamua sakata la Okwi kinyume na malalamiko yao kwani hakukuwa na lalamiko la
mchezaji huyo wa Uganda kuhusiana na malipo ya fedha zake za usajili.
Alisema kuwa cha kushangaza, kamati
hiyo ya TFF iliamua kusikiliza kesi ambayo haikuwa mbele yao na kutoa maamuzi
ambayo hata wao wameshangazwa nayo.
“Kwanza kesi yenyewe ilikuwa
haijamalizika, walituambia tuwasilishe vielelezo kuhusiana na kitendo cha
mchezaji huyo kufanya mazungumzo na klabu ya Misri, lakini cha kushangaza
maamuzi yametolewa, hili limetushangaza sana,” alisema Mapande.
Alisema kuwa mazingira yalikuwa
yameandaliwa kuibeba Simba na Okwi kwani hata malalamiko yao kwa Simba
hayakusikilizwa. “Malalamiko yetu yalikuwa wazi kabisa, yapo kimaandishi,
hatukuwai kulalamikiwa, suala la fedha za usajili la Okwi limetoka wapi, kama
lilikuwepo, mbona hatujajulishwa kimaandishi kama utaratibu ulivyo,” alisema.
Alisema kuwa Kamati hiyo kumruhusu
mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo Zacharia Hans Pope ambaye pia ni mwenyekiti
wakamati ya usajili ya Simba kuwemo katika kikao hicho kinyume na taratibu za
Fifa kupitia kifungu namba 19 kinachoeleza mgongano wa kimaslah
Mkule.blogsports.com
No comments:
Post a Comment