Pages

Ads 468x60px

Thursday, September 4, 2014

RONALDO BADO ANAWAZO LA KURUDI OLD TRAFORD.

                                                                   Cristiano Ronaldo.

Mshambuliaji wa Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo amesema  bado anatamani siku mmoja arudi kuichezea timu yake ya zamani ya Manchester United  katika siku zijazo za soka lake.
Ronaldo ambaye ni raia wa Ureno amebainisha kuwa anaipenda Manchester United  na kila mtu anafahamu hilo kwakuwa mara nyingi amekuwa akizungumza suala la kuipenda timu hiyo na mapenzi hayo yanatoka  moyoni mwake.
Pamoja na kukiri kuwa na furaha akiwa Real Madrid baada ya kudumu kwa zaidi ya miaka mine sasa tangu ajiunge nayo mwaka 2009 akitokea Man United amesema  daima anaikumbuka timu yake ya zamani kutokana na kuwa na marafiki wengi zaidi.
Licha ya Manchester United kuanza vibaya msimu huu wa ligi kuu ya Uingereza mshindi huyo wa tuzo ya mchezaji bora  dunia na ulaya kwasasa amesema usajili wa Radmel Falcao na Angel di Maria utairudisha United kwenye hadhi yake iliyozoeleka.

                         
Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment