Pages

Ads 468x60px

Wednesday, September 17, 2014

MUSTAKABALI WA UCHAGUZI WA NFF NI SEPTEMBER 20 MWAKA HUU.





Shirikisho la soka la nchini Nigeria  NFF linataraji kufanya mkutano tarehe 20 ya mwezi huu  mjini Warri kwaajili ya kupanga utaratibu wa uchaguzi kupata viongozi wapya  baada ya Fifa kutoa agizo hilo.
Kwamujibu wa katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu  nchini Nigeria Musa Amadu amesema  kikao hicho kitahudhuriwa na wawakilishi  wa vyama mbalimbali kama chama cha waamuzi,chama cha makocha na chama cha wachezaji.
Amadu amesema kikao hicho ndicho kitakachochagua  wajumbe wa kamati mbalimbali za uchaguzi huo pamoja na kupanga siku ya uchaguzi  na eneo utakapo  fanyika kabla ya  mwezi huu kumalizika.
Amadu amebainisha kuwa mkutano huo utakaojumuisha wajumbe 36 wa NFF  utahudhuriwa na mwaklishi kutoka fifa  na kila kitu kitakuwa wazi ili kuondoa wasiwasi uliyopo miongoni mwa watu juu ya utendaji wa shirikisho hilo.

                                           Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment