Pages

Ads 468x60px

Sunday, September 7, 2014

PAMBANO LA YANGA NA BIG BULLETS YA MALAWI LAOTA MBAWA.




Uongozi wa klabu ya soka ya Yanga ya jijini Daresalaam unapenda kuwatangazia Wapenzi, wanachama, washabiki na wadau wa soka kwa ujumla kuwa mechi kati ya Young Africans dhidi ya Big Bullets iliyokua ifanyike leo kwenye uwanja wa tafia  haitakuwepo.

Kwa mujibu wa waandaji wa mchezo huo chama cha soka mkoa wa Daresalaam DRFA timu ya Big Bullets imeshindwa kuwasili nchini, na jitihada za kupata timu nyingine imeshindikana.


Kwa maana hiyo Uongozi wa Yanga Africans unawaomba radhi kwa usumbufu wote ambao umejitokeza.
Daima Mbele Nyuma Mwiko.

                                 Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment