Pages

Ads 468x60px

Wednesday, September 10, 2014

YAYA TOURE :TUJILAUMU WENYEWE KWA KIPIGO CHA GOLI 4 KWA 1 DHIDI YA CAMEROON.



                                 Yaya Toure nahodha wa timu ya taifa ya Ivory Coast.

Nahodha wa timu ya taifa ya Ivory Coast Yaya Toure amewalaumu wachezaji wenzake baada ya jana  kufungwa magoli 4 kwa 1 na Cameroon kuwania kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.
Yaya ambaye ni mchezaji bora wa Afrika kwasasa  amesema pambano hilo walilocheza kwenye uwanja wa Ahmadou Ahidjo mjini Yaounde  Cameroon lilikuwa gumu lakini wao wachezaji ndio wanaopaswa kujilaumu kwa kipigo hicho cha ugenini.
Mbali na kuahidi kufanya vyema kwenye michezo inayofuata katika hatua hiyo ya makundi kufuzu kwa fainali za Afrika mwakani mshambuliaji huyo wa Manchester City amesema timu yao ilipata nafasi lakini walikosa umakini kwenye kufunga.
Ivory Coast ambayo katika mchezo unaofuata itakuwa nyumbani kuikabili Congo matokeo ya jana yamewafanya kushika nafasi ya tatu kwenye kundi lao la D wakiwa na alama 3 nyuma ya Cameroon inayoongoza kwa alama 6 na nafasi ya pili ikishikiliwa na DR Congo yenye alama 3.

MATOKEO YA MAKUNDI MENGINE MICHEZO YA JANA 10/9/14 KUFUZU AFCON 2015 .
Group A
  • Congo 2-0 Sudan
  • South Africa 0-0 Nigeria
Group B
  • Malawi 3-2 Ethiopia
  • Algeria 1-0 Mali
Group C
  • Angola 0-3 Burkina Faso
  • Lesotho 1-1 Gabon
Group D
  • Cameroon 4-1 Ivory Coast
  • Sierra Leone 0-2 DR Congo
Group E
  • Togo 2-3 Ghana
  • Uganda 2-0 Guinea
Group F
  • Mozambique 1-1 Niger
  • Cape Verde 2-1 Zambia
Group G
  • Botswana 0-2 Senegal
  • Egypt 0-1 Tunisia


                                 Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment