Senegal,Simba wa Teranga waliojiandaa kurejesha heshima yao barani Afrika.
Senegal
ilipata Uhuru wake mwaka 1960 ikiwa koloni la Ufaransa.
Kiongozi
mkuu wa nchi ya Senegal ni RAIS na hii
ni baada ya katiba ya taifa hilo iliyopitishwa
mwaka 2001 ambapo rais wa nchini
hiyo huongoza kwa miaka mitano ndipo uchaguzi hufanyika.
Rais wa sasa
wa Senegal ni Macky Sall aliyezaliwa mwaka 1961 na aliingia
madarakani April 2 mwaka 2012 akichukua
nafasi ya Abdoulaye
Wade aliingia
madarakani April 1 2000 akichukua mikoba
ya rais wa wakati huo Abdou Diouf aliyeingia matarakani January 1 mwaka 1981.
Tangu ipate uhuru
wake kutoka kwa Ufaransa mwaka 1960 Senegal imeongozwa na marais wane tuu
akiwemo huyu wasasa.
Rais wa
kwanza ambaye ni baba wa taifa la Senegal ni Léopold
Sédar Senghor
aliyeongoza kwa miaka 20 tangu sept 6
1960 hadi dec 31 1981, alizaliwa mwaka 1906 na kufariki dunia 2001 akiwa na
umri wa miaka 95.
Nchi hii inapatikana
magharibi mwa bara la Afrika na mjini
mkuu wake ni Dakar mji unaotajwa kuwa na wakazi milioni 2.45 wanaoishi jijini
humo.
Hadi dec
mwaka jana taifa hili linakadiriwa kuwa
na watu wapatao milioni 14 laki 786 mia 504,wanaume wakiwa milioni 7333 705
sawa na 49.6% ya wananchi wote huku
wanawake wakiwa milioni 7452 801 sawa na 50.4%.
Lugha kuu ya
taifa la Senegal ni Kifaransa.
Miongoni mwa
miji mashuhuri nchini Senegal mbali na jiji la Dakar ni.. Sant Louis, Ziguinchor na M'Bour.
Uchumi wa
wananchi ya Senegal unategemea
Uvuvi,kilimo cha karanga,utalii na madini aina ya phosphates, na asilimia kubwa ya wananchi wa
taifa hili ni wakulima.
Timu ya
taifa ya Senegal inajulikana kama SIMBA WA TERANGA kwa jina la utani .
Mara ya
kwanza kucheza mchezo wa kimataifa kwa timu hii ilikuwa dhidi ya British Gambia
mwaka 1959 wakati huo Senegal ikijulikana kama French Senegal.
Katika
mchezo huo Senegal ilishinda magoli 2 kwa 1 dhidi ya British Gambia ambayo
kwasasa inajulikana kama Gambia.
Ushindi
mkubwa iliyowahi kuupata Senegal ni wa magoli 7 kwa 0 dhidi ya Mouritius
ilikuwa oct 9 mwaka 2010.
Kipigo
kikubwa ilichowahi kukipata timu ya taifa ya Senegal au Simba wa Teranga ni cha
magoli 5 kwa 0 kutoka kwa Guinea march 6 mwaka 1966.
Senegal
imeshiriki kombe la dunia mara moja tuu
mwaka 2002 na kufikia hatua ya robo fainali wakati huo kikosi hicho
kikiwa chini ya kocha Bruno Metsu na kuongozwa na nahodha wa wakati huo Alhadji
Diof nyota wa zamani wa vilabu mbalimbali barani Ulaya ikiwemo Liveroop.
Bila shaka
wengi mtaikumbuka Senegali hii ambayo iliushangaza Ulimwengu kwakuifurusha Ufaransa
ya Zinedine Zidane goli 1 kwa 0 na kuwa
talk of the World.
Baada ya
ukali huo wa 2002 Senegal ikapotea kiasi cha wengi kuhoji kulikoni?ikawa hivo
baadae aliyekuwa kocha wa Senegal wakati huo Bruno Metsu akaondoka na taarifa
za kushtua zikajiri October 14 2013
kwamba amefariki dunia katika kijiji cha
Coudekerque kilichopo nchini Ufaransa .
Daima
atakumbukwa na mashabiki wengi wa Senegal kwa mchango wake alioutoa kwa timu
yao ya taifa.
Kwasasa
Senegal inashika nafasi ya 35 kwenye ubora wa soka duniani kwenye takwimu
zilizotolewa January 8 mwaka huu.
Nafasi ya
juu kuwahi kushika katika ubora wa soka duniani ni ya 26 na hii ilikuwa juni
2004 na nafasi ya chini zaidi kuwahi kushika nchi hii katika ubora huo wa soka
duniani ni ya 99 mwezi juni mwaka 2013.
Kocha mkuu
wa sasa wa timu ya taifa ya Senegal ni Alain Giresse akisaidiwa na kocha
msaidizi Aliou Cisse na nahodha wa kikosi hichi kwasasa ni Bouna Condoul ambaye
hucheza nafasi ya Golini ya Mlindamlango.
FAINALI ZA
KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA.
Senegal al
maarufu Simba wa Teranga imeshiriki kombe la mataifa ya Afrika AFCON mara 12.
Mara ya
kwanza ilikuwa 1965.
Hatua nzuri
iliyowahi kufikia kwenye fainali hizi ni
kushika nafasi ya 2 katika fainali za mwaka 2002 zilizofanyika nchini MALI na ubingwa
kunyakuliwa na CAMEROON huu ukiwa ni ubingwa wa 4 kwao.
Katika
fainali za AFCON mwaka huu Senegal ni miongoni mwa mataifa yatakayoshiriki huko
nchini Guinea ikiwa na muonekano wa tofauti kabisa na wengi walivyotarajia.
Wachezaji
wenye majina kama Demba Ba wameaachwa
kwenye kikosi hicho na badala yake chipkizi wamesheheni katika kikosi hichi
chini ya kocha mkuu Alain Giresse.
Wapo katika
kundi linaloaminika kuwa ni la kifo,kundi C lenye mataifa kama Ghana,Algeria,na
Afrika ya kusini.
Pamoja na
kuwa kwenye kundi la kifo Simba hawa wa Teranga huenda wakarejesha heshima yao
iliyopotea tangu mwaka 2002 walipotinga robo fainali ya kombe la dunia kutokana kocha wa sasa kukisuka upya kikosi
hicho huku kikisheheni nyota wengi wanaosakata soka barani Ulaya hususani
Ufaransa ambapo ni Koloni lao.
Hebu angalia
safu ya hii ya ushambuliaji wa Simba hawa wa Teranga inayoundwa na nyota
wanaotamba katika ligi kuu mbalimbali barani Ulaya hususani Uingereza hivi sasa Diafra Sakho (West Ham,
England), Mame Birame Diouf (Stoke,
England), Sadio Mané (Southampton,
England), Moussa Sow (Fenerbahçe, Turkey), Papiss Demba Cissé (Newcastle,
England), Henri Saivet (Bordeaux, France), Dame Ndoye (Lokomotiv, Russia),
Moussa Konaté (FC Sion, Switzerland)
Mimi
nakuachia wewe utafakari lakini sidhani
kama Simba wateranga wanaenda kutalii nchini Guinea mwaka huu bali wanaenda
kuweka historia nyingine mhimu katika soka la barani Afrika hivi sasa.
Mkule.blogsport.com
No comments:
Post a Comment