Pages

Ads 468x60px

Thursday, January 15, 2015

FOJARI YA UHAMISHO,FIFA YAMZUIA BEN ARFA KUREJEA KWAO UFARANSA.



                                                                Hatem Ben Arfa.
Shirikisho la soka duniani FIFA limezuia uhamisho wa mshambuliaji hatem ben arfa kutoka Hull city kwenda katika klabu ya nice inayoshiriki ligi kuu ya nchini ufaransa maarufu kama Ligi wani.

Ben Arfa raia wa ufaransa amezuiwa kuhamia katika klabu hiyo ambayo ilitangaza kumpa mkataba wa miezi 18 lakini FIFA imesema usajili huo upo kinyume na kanuni za usajili.
Shirikisho hilo imefafanua kuwa sheria za usajili haziruhusu mchezaji kusajiliwa na vilabu viwili tofauti ndani ya msimu mmoja pekee kama ilivyotokea  kwa Hatem ben arfa.
Nyota huyo mwenye mwenye umri wa miaka 27 alikua akiitumikia hull city kwa mkopo akitokea Newcastle united ambapo baada ya kumaliza muda wake na hull city Newcastle ilisitisha mkataba wake.

                                    Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment