Pages

Ads 468x60px

Friday, July 18, 2014

SERENGETI BOYS YAJIWEKA PABAYA YABANWA MBAVU NA AMAJIMBOS CHAMANZI.





                           Kikosi cha Serengeti boys.

Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 Serengeti boys leo imeshuka dimbani kuikabili Amajimbos timu ya taifa ya vijana ya Afrika ya kusini kusaka tiketi ya kucheza fainali za Afrika kwa vijana.
Pambano hilo lililochezwa kwenye uwanja wa Azam Complex nje kidogo ya jiji la Daresalam hadi dkk 90 zinamalizika timu hizo zimetoka suluhu ya kutofunga.

Baada ya kumalizika kwa mchezo huo kocha wa Serengeti Boys  Hababuu Alli Omari amesema anamatumaini kuwa watafanya vyema katika mchezo wa marejeano licha ya kwamba watakuwa ugenini.
Mchezo wa marejeano unataraji kuchezwa wiki mbili zijazo nchini Afrika ya kusini.
Hivi ndivyo vilivyokuwa vikosi vya timu zote mbili.

Kikosi cha Serengeti Boys; Mitacha Mnacha, Abdallah Jumanne/Mashaka Ngujiro dk23, Issa Baky, Adolph Mutasingwa/Kelvin Farrel dk10, Martin Kiggi, Omar Wayne, Athanas Mdam, Ali Mabuyu, Abdul Bitebo/Mohamed Mussa dk86, Prosper Mushi na Baraka Yussuf.
Amajimbos; Mondili Mpoto, Nelson Maluleke, Simon Nqoi, Notha Ngcobo, Keanu Cupido, Tendo Mukumela, Katlego Mohamme, Athenkosi Dlala, Sibongankonke Mbatha/Felix Noge, Luvuyo Mkatshana/Vuyo Mantjie na Khanyiso Nayo. 
 



                                 Mkule.blogsport.com

1 comment:

  1. Shukrani kwa kutujuza habari mbalimbali za kimichezo kila siku tupo pamoja daima Mkule.

    ReplyDelete