Pages

Ads 468x60px

Thursday, July 24, 2014

PIGO,BORIN AUMIA,DILI LA KWENDA SUNDERLAND HATARINI KUFA.





                        Faibo Borini akiwa mzigoni.

Klabu ya Liverpool inayoshiriki ligi kuu ya England imepata pigo baada ya mshambuliaji wake Fabio Borin kuumia bega katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Roma uliomalizika kwa Liverpool  kufungwa goli 1 kwa 0.

Borin ambaye aliichezea Sunderland kwa mkopo msimu uliopita  alitolewa nje katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo kutokana na kuumia bega na haijawekwa wazi ukubwa wa jeraha hilo.

Baada ya mchezo kumalizika kocha mkuu wa timu hiyo Brendan Rodgers amesema hajui kama mchezaji huyo atasalia kwenye timu hiyo msimu ujao licha ya kuendelea kuwepo na vijogoo hao wa Anfield.

Hivi karibuni zilitolewa taarifa kuwatimu hiyo imefikia makubaliano na Sunderland juu ya nyota huyo raia wa Italia kwa uhamisho wa paundi milioni 14 lakini kuumia kwa mchezaji huyo kunaweza kufanya mipango hiyo isiwepo.

                          Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment