Rais wa Tff Jamal Malinzi.
Rais wa shirikisho la soka nchini
Tff Jamal Malinzi leo amewasili mkoani Ruvuma ambapo atakuwa na mazungumzo na viongozi
wa chama cha mpira mkoani humo FARU kujadili masuala mbalimbali.
Mwenyekiti wa FARU Golden Sanga
amesema ujio wa kiongozi huyo wa ngazi ya juu kwa soka la Tanzania ni
wakihistoria na huenda ukaleta mabadiliko makubwa ya kimaendeleo.
Sanga amema mara ya mwisho kwa mkoa
wa Ruvuma kutembelewa na uongozi wa juu wa Tff ni miaka ya 1980 ambapo kipindi
hicho Tff ilikuwa inajuliakana kama chama cha soka nchini FAT na kiongozi wa
mwisho kutoka FAT kutembelea mkoa huo ni Said Elimamri.
Katika ziara hiyo ambayo ni mmoja ya
ahadi zake wakati wa kuingia ikulu ya Tff Malinzi atapata fursa ya kuzungumza
na wenyeji wake masuala mbalimbali yakimendeleo kwa soka la Ruvuma na nchi kwa
ujumla.
Malinzi anataraji kurejea Daresalaam
kesho jioni mara baada ya kufunga mashindano ya Sangawane Cup yanayofanyika
mjini Songea mkoani Ruvuma ambapo ataota zawadi kwa timu zitakazofanya vyema
kuanzia mshindi wa kwanza,wapili,watatu na wanne.
Aidha Malinzi ameahirisha safari
yake ya kwenda nchini Brazil kushuhudia fainali ya kombe la dunia hapo kesho
baina ya Argentina na Ujerumani kutokana na kubanwa na shughuli mbalimbali ya
kiutendaji katika ofisi yake.
Mkule.blogsport.com
No comments:
Post a Comment