Pages

Ads 468x60px

Saturday, July 19, 2014

JUVE YANASA SAINI YA ALVARO MORATA KUTOKA REAL MADRID.



              Alvaro Morata akiwa na jezi ya Real Madrid.

Mabingwa wa ligi kuu ya Italia Juventus wamekamilisha usajili wa mshambuliaji Alvaro Morata kutoka Real Madrid ya nchini Hispania kwa uhamisho wa Euro milioni 20 akikubali kusaini mkataba wa miaka mitano.

Morata mwenye umri wa miaka 21 jana ijumaa laiwasili  mjini Turin Italia kwaajili ya maandalizi ya kufanyiwa vipimo vya afya tayari kwakujiunga na vibibi kizee hao wa Turin.

Katika usajili huyo pande mbili zimekubaliana kuwa kutakuwa na ongezeko la kufikia Euro milioni 30 kwa Real Madrid endapo nyota huyo ataongezewa mkataba baada ya huu wa sasa.

Pia mkataba huo utaendelea kuinufauisha Real Madrid kulingana na idadi ya michezo atakayokuwa anacheza chipkizi huyo katika msimu wa 2015/2017 na 2016/2017.

Morata ambaye amefunga magoli 8 katika michezo 23 aliyocheza msimu uliopita akiwa na Reala Madrid  anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Juventus  akitokea Real Madrid baada ya kiungo Casemiro aliyekuwa kwa mkopo Fc Porto ya Ureno taarifa zilimethibitishwa leo.

                                Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment