Pages

Ads 468x60px

Thursday, July 17, 2014

PIGO KUBWA MANCHESTER UNITED,CARRICK KUKAA NJE WIKI 12.





                                      Michael Carrick.

Timu ya soka ya Manchester United itamkosa kiungo wake Michael Carrick  kwa muda wa majuma 12 baada ya kuumia kifundo cha mguu akiwa mazoezini kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu ya England unaotaraji kuanza mwezi ujao.

Taarifa ya United imesema Carrick mwenye umri wa miaka 32 amefanyiwa upasuaji leo asubuhi  na atakuwa nje ya dimba kwa majuma 10hadi 12 hivyo atakosa michezo ya mwezi wa kwanza katika msimu mpya wa ligi ya BPL.

Kuumia kwa Carrick kumethibitishwa ikiwa ni siku ya kwanza ya kazi kwa kocha  mpya wa mashetani hao wekundu Louis Van Gaal ambaye leo amezungumza na waandishi wa habari kwa mara yakwanza akiwa bosi wa United.

Akizungumzia kuumia kwa nyota huyo Van Gaal amesema ni pigo kubwa kwa timu yake kwakuwa Carrick ni mchezaji mwenye uzoefu mkubwa ambaye anahitajika kwenye kikosi chake.

                        Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment