Kikosi cha timu ya taifa ya Brazil 2014.
Hekaheka za michuano ya kombe la
dunia zinataraji kuendelea leo usiku nchini Brazil ambapo wenyeji timu ya taifa
ya Brazil watakuwa wakichuana vikali na Uholanzi katika pambano la kusaka
mshindi wa tatu.
Timu zote hizi zitakuwa zinaingia
uwanjani na maumivu yakudundwa kwenye michezo yao ya nusu fainali ambapo
Brazili ililowa mbele ya Ujerumani kwakubugizwa magoli 7 kwa 1 siku chache
zilizopita.
Brazil ambayo ilionekana kupwaya
baada ya kuwakosa nyota wake wawili mhimu kwenye pambano la nusu fainali
nahodha Thiago Silva ambaye alikuwa akitumikia adhabu ya kadi mbili za njano na
Neymar ambaye ni majeruhi leo watakuwa
wakifurahia uwepo wa Silva ambaye ameshamaliza adhabu yake.
Tayari nahodha huyo amesema watahakikisha
wanaifunga Uholanzi ili kuwafuta machozi mashabiki wao walioumia kutokana na
kipigo hicho cha kiistoria walichokipokea kutoka kwa wajerumani.
Neymar ambaye yeye ni majeruhi ataendelea
kuwa mtazamaji kutokana na kuumia uti wa mgongo.
Kwaupande wao Uholanzi chini ya
kocha mkuu Lois Van Gaan wanaingia uwanjani leo wakiwa na kumbukumbu ya
kuondoshwa kwa changamoto ya mikwaju ya matuta na Argentina kwenye pambano la
nusu fainali lililochezwa hivi majuzi.
Uholanzi ambayo ilifungwa matuta 4
kwa 2 na kikosi cha Argentina leo
itakuwa ikipigana kufa na kupona kushinda pambano hilo ili kuwapa faraja mashabiki
wake ambao wengi waliamini watarejea kumbukumbu yao ya mwaka 2010 ambapo
walifungwa na Hispania katika mchezo wa fainali nchini Afrika ya kusini.
Kikosi cha timu ya taifa Uholanzi kitakachoivaa Brazil leo.
Wakati matumaini ya Wabrazil
yakibakia kwa Oscar katika safu ya ushambuliaji, kwa upande wa uholanzi wataendelea kutegemea
majembe yao Arjen Roben na Roben van Persie na wengineo huku kiungo Wesley Sneijder
baada ya mkwaju wake kupanguliwa na mlinda mlango wa Argentina Sergio Rumero
leo atataka kufuta makosa.
Kesho pazia la michuano hiyo
iliyoanza julai 12 mwaka huu litakuwa linafungwa rasmi kwa pambano kali na la kukata
na shoka baina ya Ujerumani na Argentina kuanzia majira ya saa 4 kamili usiku
kwasaa za Afrika ya mashariki.
Kikosi cha timu ya Taifa ya Argetina kitakachoikabili Ujerumani kesho katika mchezo wa fainali ya kombe la dunia nchini Brazil 2014.
Kikosi
cha timu ya Taifa ya Ujerumani kitakachoikabili Argentina kesho katika
mchezo wa fainali ya kombe la dunia nchini Brazil 2014.
Mkule.blogsport.com
Mkule.blogsport.com
No comments:
Post a Comment